Prof. Mussa Assad leo amemkabidhi ofisi CAG mpya Charles Kichere katika ofisi ya Mkaguzi Mkuu wa Hesabu za Serikali DSM na kusema kuwa atampa ushirikiano wowote akihitaji mchango wake kwani yeye na Kichere wanafahamiana mda mrefu tangu wakati akimfundisha Chuo Kikuu cha DSM.

 

Pamoja na hayo Prof. Assad amesema 'Miaka yote napenda kupanda bamia nilisimamie liote nivune liingie jikoni nile, kwahiyo nimeingia katika kulima miezi miwili iliyopita nimewekeza sana katika kilimo ninachofikiria kwa haraka kwenda shamba kupumzika na kufanya kazi zangu za shamba wakinihitaji watu wa Mjini nitapigiwa simu nitakuja kufanya kazi, changamoto mnazijua nyingi tumepitia na unachotaka kusema nitie ukakasi na hakuna haja ya kufanya hivyo"

 

Hapo jana Novemba 4, 2019 Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. John Magufuli alimuapisha  Charles Edward Kichere kuwa Mdhibiti na Mkaguzi Mkuu wa Hesabu za Serikali (CAG).

 

Baada ya kukabidhiwa ofisi CAG mpya Charles Kichere amesema  "Tutajenga timu Profesa usiwe na wasiwasi, huwezi kufanya kazi kwa watu mliosambaratika hapo utakuwa umesambaratisha Taasisi na hutofurahi kuona mwanafunzi wako anaisambaratisha Taasisi ambayo ulikuwepo kwa miaka 5, naenda kufanya kazi kulinda mapato na nitalinda kwa wivu mkubwa sana, sitokuwa na aibu kwa watu wanaotumia mapato ya Serikali vibaya nitawaripoti, Mwalimu wangu Profesa Assad tulikutana mwaka 1994 nikiwa Chuo Kikuu mwaka wa kwanza UDSM sijawahi kupoteza mawasaliano na Profesa, kama nitahitaji ushauri Profesa nitakutafuta na hautokataaa kumpa ushauri mwanafunzi wako" 

 

 

Share with Others