Wizara ya Afya nchini Rwanda imetangaza kuchukua hatua ili kudhibiti maambukizi ya Virusi vya Corona baada ya mtu mmoja kukutwa na Virusi hivyo

Kwa muda wa wiki mbili, ibada zote zitafanywa nyumbani, shule na taasisi za elimu ya juu nazo zitafungwa, na wafanyakazi watatakiwa kuendelea na majukumu yao wakiwa nyumbani

Aidha, mikusanyiko ya sherehe na matukio ya michezo nayo imezuiwa. Wizara ya Afya imesema idadi ya watu katika mikusanyiko ya misiba inatakiwa kuwa ndogo

Biashara na migahawa itaendelea kufanya kazi lakini watu wanatakiwa kukaa umbali wa mita moja. Pia usafiri wa umma umetakiwa kuwa na idadi ndogo ya watu

Wizara ya Afya pia imetoa wito kwa wananchi kunawa mikono mara kwa mara na kuepuka kugusana

Hadi sasa, nchi 20 barani Afrika zimeripoti kuwa na maambukizi ya Virusi vya Corona huku watu Wizara ya Afya ya Rwanda imetangaza kuchukua hatua ili kudhibiti maambukizi ya Virusi vya Corona baada ya mtu mmoja kukutwa na Virusi hivyo

Kwa muda wa wiki mbili, ibada zote zitafanywa nyumbani, shule na taasisi za elimu ya juu nazo zitafungwa, na wafanyakazi watatakiwa kuendelea na majukumu yao wakiwa nyumbani

Aidha, mikusanyiko ya sherehe na matukio ya michezo nayo imezuiwa. Wizara ya Afya imesema idadi ya watu katika mikusanyiko ya misiba inatakiwa kuwa ndogo

Biashara na migahawa itaendelea kufanya kazi lakini watu wanatakiwa kukaa umbali wa mita moja. Pia usafiri wa umma umetakiwa kuwa na idadi ndogo ya watu

Wizara ya Afya pia imetoa wito kwa wananchi kunawa mikono mara kwa mara na kuepuka kugusana

Hadi sasa, nchi 20 barani Afrika zimeripoti kuwa na maambukizi ya Virusi vya Corona huku watu 157,233 wakiambukizwa na 5,844 wakifariki mpaka sasa na 75,940 wakipona kutokana na virusi hivyo 

Share with Others