Tamasha kubwa la muziki barani Afrika (Sauti za busara msimu wa 17) limeanza rasmi leo Visiwani Zanzibar katika eneo la ng'ome  kongwe likikutanisha wasanii mbalimbali kutoka kila kona barani Afrika.


Tamasha hilo linatarajiwa kudumu kwa muda wa siku nne usiku na mchana bila kusimama,na litatoa heshima kwa baadhi ya watu waliofariki hivi karibuni walioacha alama katika tasnia ya muziki barani Afrika akiwemo Ruge mutahaba ambaye alikuwa mmoja kati ya waasisi wa tamasha hilo na oliva mtukuzi aliyekuwa mwanamuziki kutoka zimbabwe.


Wengine ni Simaro Massiya Lutumba (DRC),Halikuniki(ZNZ) ,Johny Clegg(South Africa na Abdallah Matimbwa (Mbalamwezi wa the mafik band kutokea Tanzania.)


YUSUPH MAHMUD ambaye ni Mkurugenzi wa sauti za busara ameiambia mashujaa fm kuwa tamasha hilo licha ya kuwa ni la kiburudani,pia linalengo la kuitangaza Tanzania kimataifa.


Pia amesema kwa mwaka huu kupitia tamasha hilo wameamua kuja na kauli mbiu ya paza sauti pinga unyanyasaji kwakua tatizo hilo linaendelea kuathiri tasnia ya muziki hasa wanawake .


Hata hivyo,Tamasha hilo limeanza kwa maandamano yaliyoanzia mapinduzi square ambayo yamekuwa kivutio kikubwa kutokana na uwepo wa vikundi mbalimbali vya sanaa ikiwemo ngoma na sarakasi.

Share with Others