Waziri wa Ofisi ya Rais-TAMISEMI, Selemani Jafo amesema vyombo vya dola vinaendeshwa kwa kanuni na sheria zake, hivyo Serikali haiwezi kuviingilia na kuwataka wananchi kufuata sheria ili kuepuka migogoro

Jafo ameyasema hayo leo Bungeni wakati akijibu swali la Devotha Minja, Mbunge wa Viti Maalum (Chadema), ambaye ameeleza kukerwa na kauli za vitisho zinazotolewa na Jeshi la Polisi nchini kwa wananchi ambapo ndio wanaolipa kodi inayotumika kuwapa mishahara

Mbunge huyo aliitaka TAMISEMI kutoa tamko kuhusu kauli iliyotolewa na Kamanda wa Polisi wa Mkoa iliyolenga kuonya watu waliotangaza nia ya kuandamana na kusema wananchi wakiandamana wanapigwa hadi wachakazwe

Aidha, Jafo amesema "Jambo la kwanza, ni tuweke ushirikiano kila eneo, vyombo vingine vinaendeshwa kwa kanuni, hatuwezi kuingilia mambo yao ya ndani. Ni vyema wananchi wakafuata sheria ili kuondoa migongano"

Share with Others