Kamanda wa polisi mkoani Tabora Barnabas Mwakalukwa amesema kufuatia kupokea taarifa ya watu wawili kujinyonga, mwaka huu wataanza msako kuwabaini wanaotaka kujinyonga

Aidha amewakanya wanaotegemea kujinyonga kuwa tabia hizo zikome kwani wao wataanza kufanya doria na kuwakamata kabla hawajajinyonga na kisha kuwapeleka Mahakamani

Kamanda Barnaba ameongeza kuwa , “Tunaomba viongozi wa Taasisi za Kiroho wafanye doria za Kiroho za kuzima matukio ya namna hiyo kwa kutoa nasaha, elimu na Wataalamu wa Afya waende kwe wagonjwa wenye matatizo ya akili ili wawape faraja kuwa bado wana nafasi ya kuwa na maisha bora.”

Amesema wakati mwingine taifa linapoteza Wataalamu ambao wangesaidia nchi yetu na kusema “Tumepoteza Mwalimu, Mjasiriamali labda hawa baada ya miaka miwili wangekuwa Maprofesa au matajiri wa Afrika.”

Share with Others