Mkoa wa Tabora umefanikiwa kuwa mshindi wa jumla mashindano ya UMITASHUMTA 2019 baada ya timu zake kufanikiwa kufanya vizuri na kujipatia alama nyingi kuliko mikoa mingine 25 iliyoshiriki mashindano hayo mwaka huu.

Kwa mujibu wa matokeo ya washindi wa UMITASHUMTA mwaka 2019, mkoa wa Tabora umefanya vizuri katika mchezo wa goli kwa wasichana ambapo walishika nafasi ya kwanza, netiboli walishika nafasi ya pili, na kwaya walishika nafasi ya pili.

Kutokana na matokeo hayo Tabora imefanikiwa kuwa wa kwanza baada ya kujizolea jumla ya alama 153, huku nafasi ya pili ikichukuliwa na mkoa wa Dar es salaam baada ya kujinyakulia alama 147.5.

 Mkoa wa Dar es salaam umekuwa ukifanya vizuri kwa kushika nafasi ya kwanza katika kipindi cha miaka mitano iliyopita mfululizo

Nafasi ya mshindi wa tatu imechukuliwa na mkoa wa Mara baada ya kupata alama 143.7 ambazo zimetokana na ushindi kwenuye michezo ya usafi na nidhamu wavulana kwa kushika nafasi ya kwanza, riadha wasichana nafasi ya pili, mpira wa mikono wavulana na wasichana nafasi ya kwanza na soka wasichana nafasi ya pili.

Mkoa wa Mwanza ulishika nafasi ya nne ambapo timu zake zilifanya vizuri kwenye michezo ya riadha wasichana walishika nafasi ya kwanza, ngoma nafasi ya pili na soka kawaida nafasi ya tatu.

Nafasi ya tano ilichukuliwa na mkoa wa Geita, nafasi ya sita ilikwenda Mbeya, Morogoro ilichukua nafasi ya saba, Manyara ilishika nafasi ya 8, Tanga ikashika nafasi ya 9 na Mtwara ilishika nafasi ya kumi.

Mkoa wa Kilimanjaro umeshika nafasi ya 11, Dodoma 12, Shinyanga 13, Pwani 14, Kagera 15, Lindi 16, Arusha 17, Simiyu 18, Songwe 19, Kigoma 19 na 20 Kigoma.

Mikoa mingine ni Singida iliyoshika nafasi ya 21, Katavi 22, Ruvuma 23, Iringa 24, Rukwa 25 na Njombe 26

Kilele cha mashindano ya UMITASHUMTA kilihitimishwa jana katika uwanja wa Nangwanda sijaona kwa hotuba ya Waziri wa nchi Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa Mhe.Selemani Jafo
 

Share with Others