Taasisi ya kuzuia na kupambana na Rushwa (TAKUKURU) imefanya urejeshaji wa shilingi Milioni  25,480,000 kwa wakulima 152 wa ufuta waliokuwa wamedhulumiwa na viongozi wa Nachiungo na Mtunao AMCOS wilayani ya Liwale mkoani Lindi.

 

Zoezi hilo la urejeshwaji wa fedha hizo limefanywa katika kijiji cha Nangano na Brigedia Jenerali John Mbungo ambae ni kaimu mkurugenzi mkuu wa TAKUKURU ambapo amesema jamii inatakiwa kufahamu kuwa serekali ya awamu ya tano inataka haki itendeke kwa kila Mtanzania na kuhakikisha hakuna anayejihusisha na udanganyifu.

 


Sambamba na hayo Mbungo amesema mpaka kufikia Novemba 7 mwaka huu wamefanikiwa kuwashikilia viongozi 300 wa vyama vya msingi vya ushirika (AMCOS)  vilivyokuwa vinahusika katika kuwadhulumu wakulima.

 

Mbungo amesema TAKUKURU imefanikiwa kukamata mali mbalimbali za viongozi wa AMCOS pamoja na wafanyabiashara walioshirikiana nao katika mchakato mzima wa kuwaibia wakulima wa ufuta fedha zao.

 

Zoezi hilo utekelezaji wa agizo la Rais Magufuli alilotoa Oktoba 15 akiwa Kwenye Mkutano wa hadhara na Wananchi Wilayani Ruangwa mkoani Lindi

Share with Others