Wananchi wa kitongoji cha Cheketu kilichopo kijiji cha Somangasimuwilayani Kilwa mkoani Lindi wamewazuia wafanyakazi wa shirika la ugavi wa umeme TANESCO wasichimbe udongo katika maeneo ya ambayo hawajalipwa fidia.


Tukio hilo limetokea baada ya wananchi hao kuwaona wafanyakazi hao wakiingia na mitambo ya uchimbaji wa udongo huo ambapo kwa umoja waowameamua kwenda huku wakiwa na mwenyekiti wao kwa lengo la kutaka kufahamu hatma ya madai yao.

Kufuata sintofahamu hiyo Afisa mtendaji kata ya Somanga BAHAHE SHURUNGUSHWERA amefika katika eneo la tukio na kuwataka wananchi kuwa watulivu na wawaache wataalam hao waendelee na shughuli zao kwani wao hawausiki na malipo .

Pamoja na kuwatuliwa wananchi hao pia walimkaribisha meneja wa TANESCO mkoa wa Lindi SAMUEL CLIMENT ili aweze kueleza nia na madhumuni ya kufika katika eneo hilo.
 

Share with Others