Tanzania kwa kushirikiana na taasisi ya kimataifa ya uwezeshaji mifugo ya maziwa ya Land o’lakes imezindua mradi wa miaka mitano wa uzalishaji bora maziwa na kuongeza soko la bidhaa za maziwa nchini ifikapo mwaka 2025.

Akizundua mradi huo Jijini Dar es salaam, Katibu Mkuu Wizara ya Mifugo na Uvuvi Prof. Elisante Ole Gabriel amesema mradi huo unazingatia uwezeshasji kwa maafisa ugani mikoa 26 ya Tanzania bara na kwamba utaanza kutekelezwa katika mikoa minne ya Dar es salaam, Pwani, Tanga na Morogoro.

Amesema mradi huo utazingatia kuwezesha maafisa ugani, pembejeo na uzalishaji wenye tija hadi kufikia mahitaji ya soko la bidhaa za maziwa ndani na nje ya nchi.

Prof. Elisante amesema mradi huu ambao unaungwa mkono na ichi kadfha za wahjidsani ikiwemo marekani unalenga [pia luunga mkono juhudi za rais wa awamu ya tano mhe. Dk John Pombe Magufuli katika kuhakikisha nchi inakuwa katika uchumi wa viwanda na kujitegemea kiuchumi.

Amesema kwa sasa Tanzania bado ina uzalishaji mdogo wa maziwa licha ya kuwa na idadi kubwa ya mifugo huku wafugaji na sekta ya kilimo ikiabiliwa na changamoto za ugani anautaja mradi huu kuja na ufumbuzi wa wa kuhakikisha uzalishaji maziwa unaongezeka mara dufu.

Hata hivyo Prof. Elisante anawataka watanzania kupokea mradi huu kwa mikono miliwi na kuondokana na ufugaji wa k,uchunga kuelekea ufugaji wa kibiashara na kuiwesha nchi kungezea thamani bidhaa za maziwa kwa mahitaji ya ndani na nje ya nchi

Share with Others