Tume ya Uchunguzi ya Umoja wa Mataifa kuhusu Burundi imewasilisha ripoti yake mjini Geneva kuhusu ukiukwaji wa haki za binadamu nchini humo mwaka huu na mwaka jana.
Tume hiyo inashutumu ukiukaji mkubwa unaoendelea ambapo baadhi ya visa hivyo ni uhalifu dhidi ya binadamu, ikiwa ni pamoja na mauaji, watu kuuawa wakiwa mikononi mwa maafisa wa serikali, watu kutoweka, visa vya watu kukamatwa kiholela na kuwekwa kizuizini kinyume cha sheria, mateso na ukatili mwingine, unyama au udhalilishaji.
Kwa mara ya kwanza, uchunguzi wa tume ya Umoja wa Mataifa unamhusisha moja kwa moja Rais Pierre Nkurunziza kwa kutoa "wito wa kuchochea chuki na uhasama".
Kutokana na ushahidi uliokusanywa unaonesha, vijana wa chama tawala CNDD-FDD, wanahusika pakubwa katika visa hivyo, amesema Doudou Diène,ambae ni mwenyekiti wa tume ya Uchunguzi ya Umoja wa Mataifa na amebaini kwamba Rais Pierre Nkurunziza "anahusika moja kwa moja katika kuchochea chuki na machafuko".


Hata hivyo ofisi ya rais wa Burundi imekanusha madai hayo na kusem akwamba ni shutma zilizotengenezwa na baadhi ya nchi za Magharibi.


Doudou Diene amepuuzia mbali  hotuba ya Rais Pierre Nkurunziza na kusema imekua ikizingatia masuala ya kuboresha maridhiano, mshikamano wa kijamii.

Share with Others