Uhaba mkubwa wa mafuta umelikumba jiji la Nairobi Nchini Kenya huku vituo vingi vya kuuza mafuta vikiwa havina bidhaa hiyo muhimu.
Pia foleni zimeshuhudiwa nje ya vituo vichache ambavyo bado vinauza mafuta. 
Uhaba huu umesababishwa na baadhi ya wasafirishaji mafuta ambao wamesusia mafuta baada ya serikali kuongeza tozo ya asilimia 16% na wanaishinikiza serikali ya Nchi hiyo ifute kodi hiyo mpya 
Kodi hiyo ya asilimia 16 ilitangazwa na wizara ya fedha, licha ya mswada uliopitishwa na bunge ambao ulitupilia mbali kodi hiyo kwa miaka miwili iliyopita

 

Share with Others