Imeelezwa maambukizi ya virusi vya UKIMWI mkoani Lindi yamepungua kwa asilimia 3.5 kwa tafiti zilizofanywa mwaka 2018.


Hayo yameelezwa na kaimu mratibu wa ugonjwa huo Mkoani humo Dokta HAMIS AJALI ambapo amesema hali hiyo imetokana na uhamasishaji unaofanyika hasa kwa wanandoa watarajiwa ambao wanasisitizwa kupima afya zao kabla ya kufunga ndoa.

 

Nao baadhi ya wananchi wamesema licha ya maambukizi ya Virusi vya UKIMWI kupungua mkoani Lindi lakini bado kuna uzito wa vijana kujitokeza kwenda kupima afya zao.
 

Share with Others