Wakazi wa mamlaka ya mji mdogo wa Kilwa Masoko wilayani Kilwa mkoani Lindi wametakiwa kutowafumbia macho matapeli wanaojihusisha na upimaji wa maeneo wanaofahamika kama Vishoka.


Hayo yameelezwa na Afisa Mipango miji wilaya ya Kilwa HAMIS MVIGA wakati akizungumza na Mashujaa FM kutokana na vishoka kuwa changamoto na ni miongoni mwa wanaosababisha kuharibu mipango miji.

Sambamba na hilo MVIGA amewaasa wananchi wasinunue viwanja wala kuendeleza maeneo katika maeneo yaliotengwa bila kufika katika ofisi ya mipango miji ili kupata taarifa sahihi za maeneo hayo.

 

Share with Others