Wakazi wa vijiji vya Chilala, Makangala, Kinyope, Mchemi na Litipu halmashauri ya Wilaya ya Lindi wameaswa kuacha
kutembea nyakati za usiku, hususani katika maeneo ya Usharoba wa wanyama ili kuepuka madhara yanayoweza kusababishwa na wanyama pori wakali.


Kauli hiyo imetolewa na Afisa Ardhi na Maliasili wa wilaya hiyo VICTOR SHAU ikiwa ni siku chache zimepita tangu mkazi wa
Rutamba KIZITO MATEI MGOGO aripotiwe kujeruhiwa na simba watatu katika eneo la Chilala.

 

Afisa Mtendaji wa kata ya Rutamba ZAWADI RASHID NINDI amesema tukio hilo la mtu kujeruhiwa limetokea usiku wa tarehe
26 ambapo uongozi wa kata umefanikiwa kumfikisha katika zahanati ya chilala na badae katika hospitali ya Mkoa Sokoine ambapo mpaka sasa anapatiwa Matibabu.

 

 

Share with Others