Serikali ya kijiji cha Kiranjeranje kilichopo wilayani Kilwa mkoani Lindi imewataka wafanyabiashara wadogo kijijini hapo kutofanya biashara zao katika maeneo ya barabara, ili kuepuka usumbufu wa kuhamishwa.

 

Mwenyekiti wa kijiji hicho ABDALAH SAID MWAKUPETE ameyasema hayo hivi karibuni kufuatia uwepo wa malalamiko kwa baadhi ya wafanyabiashara juu ya wao kufukuzwa katika maeneo ya barabara na wakala wa barabara TANROADS.

 

Awali wafanyabiashara hao wamedai kupata usumbufu wa sehemu za kufanyia biashara kutokana na wakala huyo kuwataka kuondoka kwenye hifadhi za barabara jambo walilolitaja kuwa linaweza kuua mitaji yao.


Hivi karibuni kaimu meneja wa TANROADS Mkoa wa Lindi Mhandisi PAUL MARGWE alipokuwa akizungumza na wakazi wa kata ya Nyangao Wakati wa ziara ya Mkuu wa Mkoa huo GODFREY ZAMBI, aliwaasa wananchi kuacha matumizi mabaya ya barabara ikiwemo kufanya biashara, kulima na kujenga ndani ya hifadhi ya barabara.

 

Share with Others