Wafanyabiashara mkoani Lindi wameaswa kuwa waadilifu na kujali hali za wananchi wanyonge kwa kutopandisha bei za bidhaa katika mwezi mtukufu wa ramadhani.


Hayo yamesemwa na Shekhe Mkuu wa Mkoa wa Lindi MOHAMED MUSHANGANI katika siku ya kwanza tangu kuanza kwa mfungo huo.

Sambamba na hilo amewakumbusha waislam Mkoani humo, kutenda matendo mema na kufanya ibada hiyo itakayodumu kwa muda wa siku 30 kutegemea na muandamo wa mwezi.


Hata hivyo ,baadhi ya wafanyabiashara kutoka soko kuu la Lindi wamesema hali ya biashara ipo kawaida isipokuwa wingi wa bidhaa umepungua.

Kumekuwa na tabia ya baadhi ya wafanyabiashara wa bidhaa mbalimbali nchini kupandisha bei ya bidha katika vipindi vya mfungo na hata sikukuu 

Share with Others