Jeshi la polisi wilayani Liwale mkoani Lindi limewaonya Waganga wa kienyeji kuacha kufanya shughuli hiyo bila vibali, na kwamba
watakaobainika watafikishwa kwenye vyombo vya sheria.


Hayo yameelezwa na mkuu wa polisi wilaya ya Liwale, EDWARD MALOGO wakati akizungumza na Mashujaa FM, ambapo
amesema waganga hao maarufu kama LAMBALAMBA wanafanya shughuli hizo pembezoni mwa mji huku viongozi wa vitongoji na vijiji wakiwa hawatoi taarifa yoyote.

Sambamba na hayo MALOGO ametoa wito kwa wananchi kuacha tabia ya kwenda kwa waganga wa kienyeji wasiokuwa na vibali ili kuepukana na uhasama kati ya familia moja na nyingine huku akiwataka kutoa taarifa za siri ili kuwachukulia hatua.


Kwa upande wao wakazi wa Liwale kutoa maoni yao juu ya uwepo wa waganga wa kienyeji wasiokuwa na vibali, wakiishauri
serikali kuwachukulia hatua za kisheria.

Share with Others