Waziri wa Nchi,Ofisi ya Rais,Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa (TAMISEMI) Selemani Jafo amevitaka vyama vya siasa nchini na wagombea kuzingatia kanuni za uchaguzi wa Serikali za Mitaa ili kuhakikisha unafanyika bila ya kasoro yoyote.

Aidha amewaonya wagombea kutofanya mbwembwe au shamrashamra kama sehemu ya kufanya kampeni pindi wanapokwenda kuchukua fomu za kugombea.

Waziri JAFO ametoa onyo hilo Octoba 28 jijini Dodoma wakati akizungumza na waandishi wa habari ambapo amesema wote wenye nia ya kugombea wanapaswa kuanza kuchukua na kurejesha fomu kuanzia kesho hadi Novemba nne mwaka huu .

Pia Waziri Jafo ametoa wito kwa wasimamizi wa uchaguzi kutoingilia zoezi hilo huku akivitaka vyama vya siasa kuzingatia misingi ya kidemokrasia ikiwemo kuwadhamini wagombea wao.

Mbali na hayo amewaonya pia  wenyeviti wa mitaa na vitongoji ambao muda wao umekwisha malizika tangu octoba 22, kutokufanya jambo kinyume cha sheria.
 

Share with Others