Jamii wilayani liwale mkoani lindi imeshauriwa kutokula udongo na  badala yake watumie vyakula vinavyosaidia kuleta madini ya chuma mwilini.

 

Akizungumza na mashujaa fm mganga mfawidhi wa Hospitali ya wilaya ya Liwale DK EVARISTO KASANGA amesema wanawake wajawazito hupendelea kula udongo na ulaji huo unasababishwa na ukosefu wa madini ya chuma mwilini jambo ambalo kiafya sio vizuri na badala yake amewataka wanawake hao wale vyakula ambavyo vinaweza kuongeza madini ya chuma.

 

Aidha Dk KASANGA ameongeza kwa kusema kwamba madhara yanayoweza kujitokeza baada ya kula udongo ni pamoja na maambukizi ya vimelea vya minyoo kutokana na udongo kuwa mchafu.


Kwa upande wake mmoja wa watumiaji wa udongo Bi. ASUMINI RASHID ameelezea namna ambavyo alianza kutumia udongo kuwa ni pale tu alipopata ujauzito.

Share with Others