Wakazi wa kata ya Nangando wilayani Liwale Mkoani Lindi wamejitolea kujenga madarasa mawili ya sekondari ya Nangando ili shule hiyo ifunguliwe mwaka huu kwenye mbio za mwenge na kuanza muhula mpya wa masomo mwakani.


Wakizungumza na Mashujaa FM iliyoshiriki nao kwenye zoezi huo wakazi hao wameonesha kuwa na matumaini juu ya kukamilika kwa ujenzi huo.

 

Kwa upande wake Diwani wa kata ya Nangando JAFARI MKUNGU amewashukuru wakazi hao, huku akiwaomba kuendelea kujitokeza na kujitolea ili kuhakikisha ujenzi huo unakamilika kama walivyokusudia.

 

Nae Mkuu wa wilaya ya Liwale, SARAH CHIWAMBA ambaye ameshiriki kujitolea kwenye ujenzi huo amewapongeza wakazi wa
Nangando, huku akiwataka kukamilisha ujenzi wa maboma ya madarasa hayo kisha Halmashauri kumalizia sehemu iliyobaki.

Share with Others