Wakazi wa mkoa wa Lindi wametakiwa kujenga vyoo bora katika kaya zao ili kuepukana na magonjwa ya milipuko yanayoweza kusabishwa na vinyesi vya binadamu wanaojisaidia hovyo sehemu zisizo rasmi.

Rai hiyo imetolewa na mkuu wa mkoa wa Lindi GODFREI ZAMBI wakati akizungumza na watumishi mbalimbali wa umma wa wilaya ya Lindi, katika ukumbi wa DDC Manispaa ya Lindi.

ZAMBI amesema ndani ya manispaa ya Lindi ambako ndio mjini bado kuna wananchi ambao hawana vyoo bora na kwamba vyoo
walivyonavyo ni vya aibu.

Sambamba na hilo ZAMBI amewataka watendaji wa serikali kutimiza wajibu na kusimamia sheria ndogo ili wananchi wawe na
vyoo bora.

Share with Others