Wakazi wa kijiji cha Kitandi kata ya Mnero Ngongo wilayani Nachingwea Mkoani Lindi wameiomba serikali kufanya jitahada za upatikaji wa maji safi na salama katika kijiji hicho.


Wakizungumza na Mashujaa FM wakazi hao wameeleza kuwa tatizo la maji katika kijiji hicho ni la muda mrefu, na mpaka sasa hawaoni jitihada zinazofanywa na serikali ili kufanikisha upatikaji wa huduma hiyo muhimu.

Akitolea ufafanuzi suala hilo Diwani wa kata hiyo OMARI MBINGA amekiri kuwepo kwa tatizo hilo hususani katika kata yote ya Mnero Ngongo, huku akisema kuwa kata hiyo imepata miradi ya visima vinne kutoka shirika la GAIN lakini maji hayo bado sio mazuri kwa matumizi ya kunywa.

Diwani MBINGA amesema tayari ametoa taarifa kwa injinia wa maji wilaya ya Nachingwea ambaye wanategemea atatembelea katika miradi hiyo ili kufanya utafiti wa nini chanzo cha maji hayo kuwa machungu.

Share with Others