Wakazi wilayani Nachingwea mkoani Lindi wametakiwa kufahamu kuwa kuna wakati mashine za kielektroniki za
kukusanyia mapato (EFD) huwa zinasumbua na si kwamba watendaji wanakusudia kutotoa risiti ili wajinufaishe binafsi.

 

Hayo yameelezwa na Mtunza hazina wa wilaya ya Nachingwea MOHAMMED MNUNGUYE kwenye kikao cha
baraza la Madiwani, baada ya Diwani wa kata ya Mpiruka VERONIKA MAKOTA kuhoji juu ya watendaji kukusanya
mapato bila kutoa risiti kwa wateja.

 

MNUNGUYE ameeleza kuwa inapotokea mteja amepata huduma bila risiti anatakiwa kuendelea kufuatilia, huku
akiwataka watendaji kuweka kumbukumbu kwa wateja ambao bado hawajapewa risiti.

Share with Others