Wakulima wa korosho katika kijiji cha Shuka kilichopo Halmashauri ya Mtama leo wameanza zoezi la kupima na kupaki kwenye magunia Korosho zao katika chama chao cha ushirika cha Navanga Amcos.

 

Akizungumza kwa niaba ya wakulima wenzake AHMAD ALI ambaye pia ni mwenyekiti wa kijiji hicho amesema matarajio ya wakulima wa korosho wa shuka ni kupata bei nzuri.

 

Aidha ameishukuru serikali kwa kuendelea kuwapigania wakulima na kuiomba iendelee kuwahimiza wanunuzi kulipa fedha zao kwa wakati.

Kwa upande wake Mwenyekiti wa Navanga Amcos ALI YUSUPH amesema licha ya kuwa na mwamko mkubwa wa wakulima kupeleka kupima korosho zao ,pia wanakabiliwa na changamoto ya magunia ambapo wamepokea magunia 1200 pekee huku mahitaji yakiwa ni magunia 8000.

 

Hata hivyo katika minada wa kwanza uliofanywa na chama kikuu cha LUNALI kinachohudumia wakulima wa Ruangwa liwale na Nachingwea, wakulima wameuza korosho zao kwa Bei ya juu Tshs 2625/= na ya chini ni Tshs 2567/=

Share with Others