
Mkuu wa wilaya ya Kilwa mkoani Lindi Christopher Ngubiagai amekemea vikali nakuahidi kuwachulia hatua kali, baadhi ya wananchi wa wilaya hiyo kwa kuwazomea watalii wa kizungu na kuwaita majina ya corona baada ya watalii hao kutembelea wilaya hiyo
Ngubiagai ameyasema hayo alipokua akitoa maelekezo juu ya ugonjwa wa COVID-19 unaosababishwa na virusi vya corona ofisini kwake huku akiagiza taasisi zote binafsi na za umma wilayani humo kutengeneza sehemu ya kunawia kwa mikono watu mbalimbali pindi waingiapo ofisi zao.
Ngubiagai ameongeza kwakusema licha ya ustarabu wa wananchi wakilwa kusalimiana kwakupeana mikono nivyema kipindi hiki waepuke kusalimiana kwa kupeana mikono.
Mpaka sasa mataifa mataifa 180 yameathirika kutokana na virusi hivyo huku watu 246,594 wakiathirika na virus hivyo huku watu 10,050 wakipoteza maisha na 88,486 wakipona virusi hiyo