TAKRIBAN watu 19 wamefariki dunia hapo jana baada ya ndege ndogo ya abiria iliyokuwa ikitokea uwanja wa ndege wa kimataifa Juba kuelekea mji wa Yirol kuanguka.

Waziri wa habari Taban Abel alisema, ndege hiyo ilianguka na watu 19 wamekufa na wengine watatu wamejeruhiwa.

Alisema ndege hiyo ilikuwa imebeba abiria 22 ambapo wawili hawajulikani walipo.

pia ameongeza kwanza  mmoja wa manusura ambaye ni daktari raia wa Italia ambaye hali yake ni mbaya,  anafanyiwa upasuaji katika hospitali ya Yirol.

Kwa mujibu wa shuhuda wa ajali hiyo, ndege hiyo iliangukia katika mto na kueleza kwamba kulikuwa na miili iliyoopolewa kutoka katika mto huo.

Katika ndege hiyo kulikuwa na watoto watatu miongoni mwa abiria 22 kwa mujibu wa chanzo cha habari. David Subek, Afisa Mkuu wa Mamlaka ya Viwanja vya Ndege nchini humo alithibitisha kutokea kwa ajali hiyo

Share with Others