Hadi kufikia alfajiri ya leo, Watu 169,662 walikuwa wameambukizwa virusi hivyo huku Watu 6,518 wakipoteza maisha na Watu 77,775 wakipona

Kwa sasa virusi hivyo vimesambaa katika Mataifa 157 Duniani kote huku nchi 26 za Afrika zikiripoti Wagonjwa zikiwemo Kenya na Rwanda za Afrika Mashariki

Italia jana ilitangaza vifo vipya 368 ndani ya saa 24 na kufanya idadi ya vifo nchini humo kuwa 1,809. Wagonjwa wamefikia 24,747 huku kukiwa na Wagonjwa wapya 3,590 ndani ya saa 24

Marekani imetangaza idadi ya Wagonjwa kufikia 3,777 katika Majimbo 49 likiwemo Washighton DC na vifo vimefikia 69. Shule zimefungwa katika Majimbo 32 yakiwemo ya Los Angeles na New York City

Nchini Ufaransa Wagonjwa wamefikia 5,423 huku vifo vikifia 127. Takriban Wagonjwa 300 wamelazwa katika chumba cha Uangalizi Maalum na asilimi 50 kati yao wana miaka chini ya 60

Afrika Kusini imetangaza Ugonjwa huo kama janga la Taifa na kuzuia safari za nje ya Nchi. Kenya imezuia safari za nje ya Nchi na kufunga shule na vyuo huku Morocco nayo ikipiga marufuku safari za Kimataifa

Share with Others