Shirika la Afya Duniani (WHO) linakadiria kuwa Maambukizi mapya milioni moja ya magonjwa yanayoambukizwa kwa njia ya zinaa (STIs) hutokea kila siku ,

Hiyo inamaanisha kuwa zaidi ya maambukizi mapya milioni 376 kutokea kila mwaka yakiwemo magonjwa ya kisonono, kaswende chlamydia, na trichomoniasis,

WHO limesema kuwa ukosefu wa mafanikio ya kuzuwia kuenea kwa magonjwa ya zinaa ni moja ya sababu za kuenea kwa kasi na kuongezeka kwa kiwango hicho cha maambukizi kinamaanisha kuwa hatua za dharura za kukabiliana na maambukizi zinatakiwa zichukuliwe 

Wataalamu zaidi wanahofu juu ya kuongezeka kwa visa magonjwa ya zinaa kuwa sugu kiasi cha kutotibiwa na dawa zilizopo kwa sasa.

Zikilinganishwa na tathmini ya mwaka 2012, ripoti za WHO inasema " idadi haijapungua " katika viwango vya maambukizi mapya na yaliyopo ya magonjwa ya zinaa .

Shirika hilo la Afya Duniani linasema mtu mmoja kati ya watu 25 duniani ana walau aina moja ya maradhi ya zinaa, huku baadhi wakiwa na maambukizi ya magonjwa ya zinaa kwa wakati mmoja.

Idadi hiyo inasema kuwa mingoni mwa wagojwa waliougua  wenye umri kati ya miaka 15-49 mnamo mwaka 2016 walikuwa ni

Watu  milioni 156 walikuwa na trichomoniasis
 Watu  Milioni 127 walikuwa na chlamydia
 Wagonjwa milioni 87 walikuwa ni wagonjwa wapya wa Kisonono
 Watu milioni 6.3 walikuwa ni wagonjwa wapya wa kaswende

Share with Others