Kutoweka kwa mwandishi mpekuzi nchini Tanzania Azory Gwanda kumechukua sura mpya baada ya Waziri wa Mambo ya Nje nchini Prof Palamagamba Kabudi kusema kwamba mwandishi huyo 'alitoweka na kufariki'.

Katika mahojiano na BBC katika kipindi cha FOCUS ON AFRICA mjini London Waziri Palamagamba Kabudi amenukuliwa akisema kwamba visa vya watu kutoweka vimesababisha uchungu mwingi nchini humo.

''Wacha nikwambie unapozungumzia kuhusu kisa hicho, ni mojawapo ya visa ambavyo vimesababisha uchungu mwingi nchini Tanzania'' alisema.

Aliendelea kwa kusema, "Katika eneo la Rufiji sio tu Azory Gwanda aliyetoweka na kufariki, nataka kukuhakikishia kwamba tunachukua kila hatua sio tu katika eneo la Rufiji bali pia maeneo mengine ya Tanzania ili kuhakikisha kuwa watu wetu wako salama-sio tu waandishi , bali pia Polisi na raia wa kawaida,".

 

Azory Gwanda alitoweka toka mwaka 2017 katika wilaya ya Kibiti Mkoani Pwani 
 

Share with Others